Ticker

7/recent/ticker-posts

RAILA ODINGA ALISIFIA JESHI LA POLISI LA TANZANIA

Waziri Mkuu Mstaafu na Mwanasiasa maarufu wa Kenya ambaye aligombea pia Urais wa Kenya kwenye Uchaguzi uliopita, Raila Odinga, amewamwagia sifa Polisi wa Tanzania kwamba wanajali utu na wana utulivu na usikivu pale wanapotekeleza majukumu yao kama ilivyo kwa Polisi wa Ulaya.

Akiongea Kanisani leo March 26,2023 wakati wa Ibada iliyofanyika eneo la Embakasi, Odinga amenukuliwa akisema “Kule Tanzania Mwl. Nyerere aliwafundisha Askari walipopata Uhuru, Askari wakapelekwa Shule maalum ya kuwafanya Watu hao kuwa Binadamu kutumia utu, kwahiyo kule Tanzania Askari akitaka kukushika anakuambia ‘Ndugu naomba nikushike’ ukimwambia kuna kitu nafanya atakuambia endelea, ukimaliza atakuambia ni kosa gani umefanya”


"Ni kama Ulaya kama unatembea umepotea njia unakwenda kwa Polisi unamwambia Afande unaweza kunionesha njia kwenda sehemu anakuonesha na ukimwambia Asante sana, anakupigia na saluti”

"Kuja Nairobi hapa, hapa wewe umetoka nje ya Nairobi umekuja kwa basi halafu haujui Barabara inayoelekea Kariakoo, uende kwa Polisi umwambie ‘Afande nimepotea nioneshe njia ya Karikaoo’ atakuuliza ‘umepotea naomba kitambulisho’ ooh kitambulisho niliacha nyumbani, anakuambia huna kitambulisho, unapigwa pingu unaenda Mahabusu kesho Mahakamani unashtakiwa.

Post a Comment

0 Comments