Ticker

7/recent/ticker-posts

RUTO AKARIBISHA MAZUNGUMZO YENYE KUJALI MASLAHI YA KENYA


 

Rais Ruto

RAIS wa Kenya William Kipchirchir Samoei Arap Ruto amesema kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga kwa maslahi ya Kenya na wananchi wake.

 Ruto ameweka wazi kuwa atakuwa tayari kufanya mazungumzo hayo kwa mujibu sheria na Katiba ya Kenya ili kutafuta mustakabali mzuri wa taifa lao.

Amesema haoni sababu ya Ruto na wafuasi wake kuandamana na kutaka kuleta machafuko ambayo yatairudisha Kenya kwenye mkwamo, hatakubaliana na hali hiyo.

“Niko tayari kuingia kwenye mazungumzo na kiongozi yeyote yule kama tunataka kuzungumzia maendeleo na mustakabali wa taifa, njia sahihi za kupita na namna gani tutapambana na changamoto zinazowakabili wananchi wetu. Nitafanya mazungumzo yenye kuheshimu sheria na katiba.” Amesema Rais Ruto wakati wa maombi yaliyofanyika Kapsabet County ya Nandi. 

Post a Comment

0 Comments