Ticker

7/recent/ticker-posts

MKUU WA WILAYA ATENGULIWA USIKU MWINGI


Taarifa ya Ikulu

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga,  Jane Nyamsenda na nafasi yake kujazwa na Sixtus Mapunda.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunusi, uteuzi wa Mapunda umeanza mara moja.

Wadadisi wa mambo wanaamini kuwa moja ya sababu zilizoonekana kuchangia kutumbuliwa kwa Nyamsenda ni kitendo chake cha kushiriki kwenye igizo la shambulizi la kutaka kumuua kiongozi wa juu wa nchi alilolifanya wakati wa kilele cha siku wa wanawake duniani wilayani humo.

Post a Comment

0 Comments