Ticker

7/recent/ticker-posts

MKONO WA BWANA KUONEKANA TAMASHA LA PASAKA DAR

  

 

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama kulia, akiongea na waandishi wa Habari ambao hawapo pichani.

KUNDI LA muziki wa injili la Zabron la nchini Tanzania, linatarajiwa kuuonesha mkono wa bwana kwenye Tamasha la pasaka linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders Aprili 9 mwaka huu.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Promotion ambaye pia ni mwandaaji wa tamasha hilo,  Alex Msama amesema tamasha litakua la aina tofauti kwa kuwa waimbaji wote wataimba mubashara na hakuna kiingilio.

“Kuna wasanii wengi wakubwa wa muziki wa Injili kutoka nje watakuwepo, kuna ambao hawajawahi kufika Tanzania, ndio itakua mara ya kwanza kutumbuiza, “ amesema Msama.

Amesema kwa sasa wameanza kuweka mambo sawa kuhakikisha tamasha hilo pendwa linafanyika kwa ubora na kishindo kikubwa.

“Wapenzi na washabiki wa nyimbo za Injili wakae mkao wa kuzikosha nafsi zao, huku wakimtukuza Mungu kwa nyimbo za Injili.

”Tulikuwa kimya kwa muda mrefu kwa sababu mbalimbali, lakini kwa sasa tumeamua kurudi upya na tamasha letu pendwa la Pasaka, ” amesema Msama.

 

 

 

 

 


 

 

 

Post a Comment

0 Comments