Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikainao wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.
Stergomena Tax amewataka Watanzania wote waishio nje ya nchi kufuata sheria,
kanuni na taratibu za nchi walizopo ili kulinda taswira yaTanzania.
Dkt. Tax alitoa rai hiyoleoJijini Dar es Salaam
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya taarifa za kifo cha Mtanzania aliyefariki dunia nchini Urusi ndugu Nemes Tarimo.
Marehemu Nemes Tarimo |
Amefafanua kuwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania,
Mtanzania yeyote haruhusiwi kujiunga na Jeshi la nchi yoyote duniani zaidi ya Jeshi la
Wananchi wa Tanzania kwa kufuata taratibu zilizopo.
“Nitoe rai kwa Watanzania kuhakikisha wanazingatia sheria
kanuni na taratibu za nchi walizopo, na pia wawe mabalozi wazuri wakulinda taswira ya
Tanzania. Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa sheria zetu, Mtanzaniayoyoteharuhusiwikujiunganajeshi
la nchiyoyoteisipokuwaJeshi la Tanzania nakufanyahivyonikuvunja sheria.”
Akifafanua suala la Tarimo amesema
Mtanzania huyo alikwenda nchini Urusi mwaka 2020 kwa lengo la kujiunga na Chuo Kikuu
cha Moscow Technological University (MIREA) kwa masomo ya Shahada
ya Uzamili katika fani ya Business Informatics.
Ameongeza kuwa Mwezi Machi 2022,
Mtanzania huyo alitiwa hatiani kwa kuhusika na vitendo vya uhalifu na kwa mujibu wa Sheria
za Urusi alihukumiwa kifungo cha miaka saba (7) gerezani.
Waziri Tax ameongeza kuwa Bw.
Tarimo akiwa gerezani alijiunga na kikundi binafsi cha kijeshi cha Wagner kilichopo nchini humo na kuahidiwa kulipwa
fedha na kuachiwa huru baada ya kumalizika kwa vita jambo alilolikubali na kujiunga na kikundi hicho,
ambapo alipelekwa nchini Ukraini kupigana na hatimae mauti yalimkuta huko.
Dkt. Tax amesema kuwa mwili wa marehemu umeondoka nchini Urusi tarehe 24
Januari 2023
na unatarajiwa kuwasili nchini muda wowote kuanzia sasa na kuongeza kuwa Serikali imekuwa ikiwasiliana na Serikali ya Urusi ili kuhakikisha mwili wa Marehemu Tarimo unarejeshwa nchini na kukabidhiwa kwa familia yake kwa ajili ya taratibu
za mazishi.
Mhe. Waziri ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu,
jamaa na Watanzania kwa jumla kufuatia msiba huo.
Dkt. Tax ameuhakikishia umma na Diaspora
wa Kitanzania wakiwemo wanafunzi walioko masomoni duniani kote kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano wakati wote.
0 Comments