Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU WA ZAMANI IKULU CHAMWINO

Rais Samia Suluhu Hassan leo Februari 3,2024 amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya (Waziri Mkuu wa 3 wa Tanzania), Ikulu ya Chamwino . 

Waziri Mkuu mstaafu Msuya aliungana na Rais Samia katika ununuzi wa hisa zaidi kutoka kwa mwekezaji ili kutekeleza nia ya kuongeza umiliki wa serikali katika kitalu cha gesi asilia cha Mnazi Bay.  

Rais Samia anasema: Mabadiliko ya tabianchi yamefanya mahitaji ya gesi na nishati nyingine mbadala kuwa kipaumbele katika kujenga uchumi shindani hivyo basi, kama nchi hatuna budi kuongeza uzalishaji na usambazaji.  

 "Lengo la kila Mtanzania ni kuona rasilimali za nchi ikiwemo gesi asilia zinawanufaisha wananchi na Taifa kikamilifu.
 "Matarajio yangu na ya kila Mtanzania ni kuona watu wote tunaowapa dhamana ya kusimamia mashirika na taasisi za kutekekeleza malengo yetu kama Taifa wanaelewa matarajio yetu, wanaelewa wanapaswa kufanya kazi kwa ubunifu na weledi wa hali ya juu, na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa letu, na si vinginevyo."

Post a Comment

0 Comments