Ticker

7/recent/ticker-posts

PRUDENCIA KIMITI AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA

Pru Kimiti alipokabidhiwa tuzo ya MBE

NA JIMMY KIANGO,AFRINEWSSWAHILI,  DSM

Prudencia Paul Kimiti, mtoto wa mwanasiasa na Waziri wa zamani wa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Paul Kimiti anashiriki kikamilifu kuitangaza  nchi yake kimataifa ndani ya Uingereza.
Prudencia maarufu kama Pru ni  Mtanzania wa kwanza na pekoe hadi sasa kutunukiwa  tuzo ya heshima ya Member of the  Most Excellent Order of the British Empire (MBE).
MBE ni tuzo yenye heshima kubwa ambayo hutolewa kwa raia wa Uingereza waliofanya mambo makubwa kwa kuyoa  mchango kwenye jamii na mara nyingi ni watu maarufu ndio hupata tuzo hii nchini Uingereza.

Hata hivyo Pru ameipata tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika maeneo yake ya kazi.Prudencia ni Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi katika mamlaka ya mapato na ushuru nchini Uingereza HMRC na amekuwa akihusika pia kutetea haki za walio wachache (minorities).

Alikabidhiwa  tuzo hiyo mwishoni mwa  mwaka 2023 na Anne, Princess Royal, mtoto wa pili na wa kike pekee wa hayati Malkia Elizabeth II na Prince Philip, Duke of Edinburgh. Anne ni dada yake Mfalme Charles III.

Hafla hiyo ilifanyika kwenye Ikulu ya Windsor na  ilihudhuriwa pia na wazazi wake, akiwemo baba yake Mzee Paul Kimiti.

Kwenye mahojiano yake yaliyofanyika Januari 7,2024 na Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC), Pru alisema  tuzo hiyo imesaidia kutangaza Tanzania kwa kiasi kikubwa.

"Nimesaidia kuitangaza Tanzania kwani sasa wanaamini kuwa Tanzania kwenye maeneo mbalimbali."

Prudencia anasema aliamua kujiingiza katika harakati za kutetea haki za watu walio wachache nchini humo baada ya yeye mwenyewe kukumbana na ubaguzi wakati alipokuwa akitafuta kazi.

Prudencia alihamia nchini Uingereza mwaka 1996 alikoenda



Post a Comment

0 Comments