Ticker

7/recent/ticker-posts

MO SALAH, SADIO MANE WAKOSA MAKALI AFCON

KINARA wa magoli kwenye michuano ya kombe la Mataifa Afrika AFCON 2023 sio Mo Salah, Victor Osimhen, Sadio Mane, Inaki Williams wala Nicolas Jackson. Emilio Nsue wa Guinea ya Ikweta ambaye kiasilia anachezea nafasi ya beki wa kulia katika klabu ya CF Intercity ya Ligi daraja la tatu Uhispania ndio kinara wa magoli AFCON 2023 akiwa na magoli matano. 

 Nsue ambaye pia anamudu kucheza kama winga wa kulia amefunga magoli matano kwenye AFCON 2023 yakiwemo hat-trick dhidi ya Guinea Bissau na magoli mawili leo dhidi ya wenyeji, Ivory Coast. Laurent Pokou ndio mchezaji pekee aliyewahi kufunga magoli mengi zaidi (7) kwenye hatua ya makundi ya michuano ya AFCON kumzidi Nsue mwenye mwenye matano. 

 MSIMAMO WA MAGOLI AFCON 2023 🇬🇶 Emilio Nsue —5 🇩🇿 Baghdad Bounedjah—3 🇸🇳 Lamine Camara—2 🇬🇭 Mohammed Kudus—2 🇧🇫 Bertrand Traore—2 🇿🇦 Themba Zwane— 2 🇪🇬 Mostafa Mohamed—2

Post a Comment

0 Comments