Ticker

7/recent/ticker-posts

TANZANIA BADO INAMALENGO NA AMROUCHE

Waziri mwenye dhamana ya michezo nchini Dkt. Damas Ndumbaro ameweka wazi kuwa bado wapo na kocha mkuu Adel Amrouche hadi adhabu yake itakapotamatika. Dkt. Ndumbaro amesema kuwa Adel amefanya makubwa na ndiye aliyeifikisha timu kwenye michuano ya AFCON inayoendelea huko nchini Ivory Coast hivyo watakuwa nae katika changamoto anazopitia na hawatasitisha mkataba wake. “Bado sisi kama Serikali ambao ndio walipa mshahara ukiadhibiwa sio muda wa kumzodoa, tupo naye kwenye kipindi hiki kigumu anachopitia”. “Bado tuna imani na mwalimu, yeye ndiye ametufikisha hapa sehemu ya kufuzu, Mwalimu huyu ndiye ametengeneza timu hii, tupo na mwalimu, hatujasitisha mkataba, ameadhibiwa na CAF, hajaadhibiwa na serikali wala TFF”. “Sisi katika kipindi hiki kigumu ambacho mwalimu ana kipitia tuko nae na tutaendelea kuwa nae, kumpa sapoti yote ambayo inahitajika, ili yeye apite kwenye kipindi hiki kigumu kwa salama kabisa”. Kwasasa Stars ipo chini ya kocha wa muda Hemed Suleiman ambaye anasaidiwa na mshambuliaji wa zamani wa Stars Juma Mgunda. Jumatano hii Taifa Stars ya Hemed Morocco itaenda kutupa karata yake ya mwisho hatua ya makundi dhidi ya DR Congo.

Post a Comment

0 Comments