Ticker

7/recent/ticker-posts

MBAPE AWEKEWA MKWANJA MREFU ZAIDI PSG

Uongozi wa Klabu Bingwa nchini Ufaransa ‘Paris St-Germain’ unadaiwa kumuwekea mezani mshambuliaji wao, Kylian Mbappe ofa ya mkataba wa mwaka mmoja ambao utamuwezesha kupata Euro 100 milioni kwa msimu. Mbappe anadaiwa kuwa kwenye mpango wa kutaka Real Madrid katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi, hivyo mabosi wa PSG wanapambana kutaka kumbakisha. Kiasi hicho cha pesa ambacho PSG imekiweka mezani, kinadaiwa kuwa ni mara tatu ya kile ambacho Madrid imeahidi kumpa ikiwa atajiunga nayo mwishoni mwa msimu huu. Madrid inataka Mbappe afanye uamuzi kabla ya mwezi huu kuisha ili kujua ikiwa atakubali kujiunga na timu yao mwishoni mwa msimu kwa mshahara unaodaiwa kuwa ni Euro 30 milioni kwa mwaka. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, msimu huu amecheza mechi 25 za michuano yote na kufunga mabao 26. Ingawa Madrid imemuahidi mshahara huo ripoti zinadai huenda akapewa bonasi kubwa ambazo zitamfanya kupata pesa nyingi zaidi.

Post a Comment

0 Comments