Ticker

7/recent/ticker-posts

MOURINHO AJIVUNIA XABI ALONSO

Kocha José Mourinho alipoulizwa kuhusu kocha anayechipukia Xabi Alonso alisema ‘’ alifundishwa na Guardiola, nikamfundisha mimi, akapita kwenye mikono ya Ancelotti, na Benítez kwanini asiwe kocha bora duniani.’’ 

Xabi Alonso ni tatizo jipya sio tu pale Ujerumani ni tishio hadi huku Duniani hana majina makubwa sana pale Bayern Leverkusen lakini kupata alama 3 mbele yake ni mfupa uliowashinda wengi pale Ujerumani na hata ulaya kwa ujumla Kulikuwa na dalili za leo kupoteza ugenini kwa RB Leipzig baadae akageuza upepo kuwa sare Wakati wakazi wa miji ya mbali kama Bonn wakiondoka uwanjani Red Bull Arena Leipzig kurejea makwao takribani kilometa 497 wakijua tayari Alonso ameambulia saree jionii kabisa anapata alama 3. 

Hadi sasa ameiongoza Leverkusen michezo 27 ndani ya msimu huu katika mashindano yoote na hajapoteza mchezo hata mmoja anaikaribia rekodi ya Bayern Munich ya kucheza michezo 32  Bayern Munich (2019-2020), mechi 27 - Werder Bremen (2003-2004) mechi 27 - Bayer Leverkusen (2023 hadi sasa Alonso anahitaji michezo mitano atembee katika rekodi ya Bayern Munich.

Post a Comment

0 Comments