Ticker

7/recent/ticker-posts

NEC YATAMBUA MCHANGO WA WADAU KWENYE CHAGUZI ZAKE

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) imesema inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wadau wa uchaguzi katika kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na ushirikiano katika kutoa elimu ya mpiga kura.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi kuhusu majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura leo tarehe 17 Novemba, 2023 jijini Dar es Salaam.


Jaji Mwambegele amesema uboreshaji huo utafanyika kwenye Kata ya Ng’ambo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora na Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara kuanzia tarehe 24 hadi 30 Novemba, 2023.

Wadau hao wa uchaguzi wanajumuisha Viongozi wa Dini, Asasi za kiraia, Wahariri wa vyombo vya habari, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Vijana. Mkutano huo umefanyika siku moja baada ya Tume kukutana na viongozi wa vyama vya siasa kwa dhumuni la kuwajulisha kuhusu uboreshaji huo.

Post a Comment

0 Comments