Ticker

7/recent/ticker-posts

MAMA WA KAMBO AFANYA UKATILI KWA WATOTO WAWILI

Watoto wawili wa familia moja, Dickson Zakaria (5) na Goodluck Zakaria (4) wamefariki baada ya mama yao wa kambo kudaiwa kuwanywesha dawa ya kuulia wadudu kwenye mazao.

Akizungumza Agosti 14, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema tukio hilo linadaiwa kutokea Agosti 12, 2023 saa tatu usiku katika kijiji na kata ya Itobo Wilaya ya Nzega.

Amesema watoto hao walidaiowa walikorogewa sumu na mama huyo (jina limehifadhiwa) kisha nayeye kunywa sumu hiyo.

Abwao ametaja chanzo cha tukio hilo ni baada ya baba wa watoto hao aitwaye Zakaria Dotto kudaiwa kutotoa fedha za matumizi na kusababisha mzozo kati yao.

Kitendo hicho kinadaiwa kumuudhi mama huyo aliyeamua kukoroga sumu ya dawa ya kuulia wadudu kwenye mazao na kuwanywesha watoto hao na yeye kuinywa.

Post a Comment

0 Comments