Ticker

7/recent/ticker-posts

DAR ES SALAAM KUFUTA SHULE ZA KUTWA


​Katika kudhibiti nidhamu kwa wanafunzi wa shule za Sekondari, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wapo kwenye mchakato wa kufuta shule za kutwa.

Chalamila, ameyasema hayo leo Agosti 14, 2023 katika uwanja wa shule ya Sekondari ya Azania kwenye hafla ya awamu ya Tano ya  kukabidhi magari kwa Maafisa Elimu wa Sekondari kwa  Halmashauri  nane.

Amesema,  Mkoa  wa Dar es Saalam una shule za sekondari 182 na za binafsi zipo nyingi zaidi ya 200.

"Katika Mkoa tunapokea sh billion 1.3 fedha zinazohudumia wanafunzi kama ada na posho ya madaraka kwa walimu.

Amesema, pamoja na kwamba Dar es Salaam ina shule nyingi,  kidato cha sita ndio  inafanya vizuri lakini kidato cha nne bado ni changamoto kwa sababu kuna shule nyingi sio za bweni.

"Na kwa sababu ya vitendo vingi vinavyoendelea mitaani ikiwemo ukosefu wa maadili, foleni,  pamoja na changamoto nyingine,  sisi tumeshakaa kikao chetu na shule zetu, tumepanga mipango kwamba sasa tujipe muda tuanze kufuta shule za kutwa ili hapa katikati kote tuwe na shule za bweni tu.." Amesema Chalamila na kuongeza

 "Tutafuta shule za kutwa tubaki na Bweni hii itasaidia kumanage nidhamu ya wanafunzi katika makuzi yao lakini pia muda wanaofika shule na hata walimu wa ziada ni rahisi kuweza kuwamanage wanapokuwa pamoja.

"Tutakuletea 'concept' mezani  mh Waziri ( Angela Kairuki - Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi) kwako ili kama kuna wafadhili basi wafikirie pia Mkoa wetu, si tu kuwa na shule nyingi  ni kwamba una wanafunzi pia wengi." Amesema

Post a Comment

0 Comments