Ticker

7/recent/ticker-posts

SERIKALI YA SIERALIONE YAKWAMISHA JARIBIO LA MAPINDUZI

SIERRA LEONE

Baada ya mapinduzi ya Niger, Sierra Leone nako kuna jambo. Mwanzoni mwa mwezi Agosti watu zaidi 10 wamekamatwa nchini Sierra Leone kwa njama ya kupanga mapinduzi ya kumpindua Rais Julius Maada Bio (kulia). Mkuu wa jeshi la Sierra Leone, Lt. Gen. P.K. Lavahun (picha ya kushoto) aliwataka askari kuwa waadilifu kwa serikali, ni baada ya IGP, William Sellu, wq Sierra Leone kutoa tangazo la kukamatwa watu hao kwa kosa tajwa.

Kati ya waliokamatwa kwa njama za kupanga mapinduzi hayo ni maafisa nane wa jeshi, sita wa jeshi la polisi, na afisa mstaafu mmoja wa jeshi la polisi.

Rais wa sasa wa Sierra Leone alikuwa mwanajeshi na alikuwa miongoni mwa waliompindua Rais Joseph Momoh, 29 April 1992, na Valentine Strasser akawa Rais mpya chini ya umri wa miaka 30. Akautumia ujana Ikulu kufidia shuluba aliyoipata vitani wakati wakipigana na waasi wa RUF (Revolutionary United Front) wakiongozwa na gwiji wa mapigano kamanda Foday Sanko chini ya "Operation Pay Yourself." Filamu ya The Blood Diamond imetokana na hadithi ya suala hilo.


Baada ya Valentine Strasser kuitumia vibaya Ikulu, Julius Maada Bio akampindua na yeye kuwa Rais akiwa na nia ya kuifanya Sierra Leone kuwa nchi ya kidemokrasia badala ya kijeshi. Strasser alikimbia nchini.

Kwa sasa Julius Maada Bio ni Rais kwa kuchagukiwa na wananchi.

Jalimu.

Na Kizito Mpangala ....

Post a Comment

0 Comments