Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema hadi kufika Jumanne ya Julai 18,2023 watakuwa wamemaliza zoezi zima la utambulisho wa usajili wao, lakini kwa sasa bado hawajamaliza. "Watu wanafikiri utambulisho wa Jonas Mkude ndio namba 6 tuliyoisema, bado namba sita hajatangazwa"
Alisema mchezaji atakaevaa jezi namba 6 atakuwa ni mtu wa mwisho kutangazwa na siku akitangazwa wananchi wataingia mtaani kufurahia kwani itakuwa ni kama sikukuu ya mwaka mpya.
"Tukimtambulisha, mafataki yatapigwa, ngoma zitapigwa, nyimbo zitaimbwa kila pande ya nchi hii watu watafurahi"
"Tutamtambulisha kabla ya wiki ya Wananchi na Kaizer Chiefs wao ndio watakuwa watu wa mfano kuwasimulia watu wengine kuhusu unyama na ukatili alionao huyu jezi namba 6,"alisema Kamwe.
Yanga inatarajia kumenyana na Kaizer Chiefs kwenye siku ya Mwananchi.
0 Comments