Kiungo fundi wa mpira, Mzambia Clatous Chota Chama, ameamza usumbufu ndani ya klabu ya Simba.
Chama hajasafiri na kikosi cha Simba kilichopo nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa.
Imeelezwa kuwa pamoja na kudaiwa kuwa na matatizo ya kifamilia, lakini mchezaji huyo ambae yupo Tanzania, hajasafiri kwa sababu za kimaslahi na kwamba ameuomba uongozi kumboreshea maslahi yake au kumruhusu aondoke.
Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula amenukuliwa Leo Asubuhi akisema kuwa kiungo huyo ana matatizo binafsi.
Zipo taarifa kuwa mkataba wa Chama na Simba SC umesalia mwaka mmoja na kwamba ameuambia uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi kuwa anahitaji maongezi na ana ofa mkononi lakini alipoambiwa aseme ofa inatoka wapi Hata hivuo amesema OFA hizo ni siri.
0 Comments