Ticker

7/recent/ticker-posts

YALIYOJIRI WAKATI WA UWASILISHWAJI WA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA HUDUMA ZA HABARI, JUNI 13, 2023 BUNGENI JIJINI DODOMA

YALIYOJIRI WAKATI WA UWASILISHWAJI WA MAREKEBISHO YA  SHERIA ZA HUDUMA ZA HABARI, LEO JUNI 13, 2023 BUNGENI JIJINI DODOMA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi

Kifungu cha 5 kinapendekezo kufanyiwa marekebisho kwa lengo la kumuondolea Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Habari jukumu la uratibu wa matangazo yote ya Serikali, na pia kuiwezesha Serikali kuwa na uhuru wa kuchagua chombo cha habari kitakachokitumia kwa ajili ya matangazo kwa kuzingatia nguvu ya ushindani katika soko.

Aidha, inapendekezo kufanyia marekebisho kifungu cha 38 kwa madhumuni ya kuongeza haki ya uhuru wa maoni.

Muswada unapendekeza marekebisho kwenye kifungu cha 50, 51, 53, 54, 55, 63 na 64 kwa madhumuni ya kupunguza adhabu kwa makosa yatokanayo na ukiukwaji wa sheria hii, kuwafanya Wanahabari kujirudi na kufurahia kazi zao.

Mapendekezo ya marekebisho ya vifungu hivyo yanakusudia kuondoa adhabu kwa wamiliki wa

mitambo ya uchapishaji, ambao katika hali ya kawaida, hawana uwezo wa kudhibiti maudhui yanayochapishwa katika mitambo hiyo ya uchapishaji.

Maoni na Ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari

Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Florent Laurent Kyombo

Kamati ilielezwa kuwa marekebisho yanayopendekezwa katika sehemu hii yanalenga kumwondolea Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Habari, jukumu la uratibu wa matangazo yote ya Serikali, na pia kuiwezesha Serikali kuwa na uhuru wa kuchagua chombo cha Habari itakachokitumia kwa ajili ya matangazo, kwa kuzingatia nguvu ya ushindani katika soko kwa kufuta aya (I) ya kifungu cha 5.

Aidha, Muswada unapendekeza kufutwa kwa kifungu 38(3) cha Sheria ya Habari kilichoweka masharti ya mtu kushtakiwa kwa makosa ya kijinai ama madai pale anapochapisha taarifa zinazodhaniwa kuwa na uhuru

usioweza kuingiliwa (absolutely priviledged) kwa madhumuni ya kuongeza haki ya uhuru wa maoni.

Vilevile Muswada unapendekeza marekebisho kwenye vifungu vya 50 hadi 55 na vifungu vya 63 na 64 kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba wanahabari wanafurahia haki yao ya uhuru wa maoni, haki ya kupata Habari na uhuru katika kazi zao za uhariri bila kuwa na woga wa adhabu za kijinai. 

Mapendekezo hayo, Pamoja na mambo mengine, yanalenga kuwaondoa wanahabari katika makosa yanayohusiana na kashfa za kjinai, makosa mabayo kwa kawaida yanaangukia katika utaratibu wa mashauri ya madai. Aidha, mapendekezo ya marekebisho ya vifungu hivyo yanaenda sambamba na kuondoa adhabu kwa wamiliki wa mitambo ya uchapishaji, ambao katika hali ya kawaida hawana uwezo wa kudhibiti maudhi yanayochapishwa katika mitambo hiyo ya uchapishaji.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye

Mhe. Rais ndio aliyeagiza mapitio ya Sheri ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, namshukuru sana Mhe. Rais kwa uamuzi wake huo.

Hoja 8 kati ya 21 tukakubaliana zibaki kama zilivyo, laki hoja zingine tukakubaliana zifanyiwe marekebisho, ikiwemo kufutwa.Katika sheria hii tumeondoa jinai kabisa. Hili ni jambo zuri litaijenga Tasnia ya Habari ikue na kuendelea vizuri.

Baadhi ya mambo tulikubaliana kwamba yaende kurekebishwa au kufanyiwa kazi kwenye kanuni tutakazozitunga hivi karibuni, na mojawapo ni suala la leseni na muda wa leseni.

Kwenye sheria hii, tumezingatia haki za walaji wa kazi za Wanahabari, maana nao wana haki yao. Kwanza kupewa taarifa ambazo ni sahihi, na ndio maana kwenye sheria hii tunataka taaluma ya habari iwe taaluma, ili waingie watu wenye weledi, wachakate taarifa vizuri, wawalishe watumiaji wa taarifa zao jambo ambalo limechakatwa kitaalam.

Tunazo taasisi za kimataifa, ambazo zinafanya tathmini ya hali ya demokrasia, Uhuru wa Wanahabari na Uhuru wa Kujieleza. Naziomba taasisi hizi zitumie taarifa za sasa hivi, baada ya mabadiliko haya watufanyie tathmini. Maana wamekuwa wakitumia taarifa za muda mrefu, kwa hiyo inaonekana kama hatujapiga hatua wakati Serikali ya Awamu ya Sita imefanya mengi katika kurekebisha uhuru wa watu kujieleza, uhuru wa Wanahabari na kupanua wigo wa demokrasia.

Imeandaliwa na Idara ya Habari - MAELEZO

Post a Comment

0 Comments