Mabingwa mara 29, soka Tanzania Bara Yanga, Leo wamepata mapokezi ya kifalme yaliyolitikisa Jiji la Dar es Salaam.
Katika mapokezi hayo bodaboda wameonekana kwa wingi huku wakiimba nyimbo mbalimbali za kuisapoti timu hiyo baada ya kutwaa taji hilo.
Mbali na madereva wa Bodaboda pia maelfu ya mashaiki walijitokeza Kwa wingi kwenye gwaride la Yanga la kusherehekea ubingwa wa 29 wa Ligi Kuu Bara.
Hata hivyo katika mapokezi hayo bodaboda wameonekana kwa wingi huku wakiimba nyimbo mbalimbali za shangwe.
Mashabiki hao wa Yanga walionekana katika maeneo ya Vingunguti ambapo gwaride hilo lilipita na kuendelea kwenda hadi Jangwani. Mashabiki hao wamejitokeza huku wakiwa wamevalia jezi za Yanga pamoja na kuimba na kupiga mavuvuzela.
Yanga imetua leo jijini Dar es Salaam ikitokea Mbeya ilikohitimisha msimu wa Ligi Kuu jana na kukabidhiwa taji hilo.
Pamoja na ushindi wa 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons, Yanga ilishanyakua ubingwa Ikiwa na michezo miwili mkononi.
0 Comments