HALI YA RAIS MUSEVEN YAIMARIKA
Hali ya Rais wa Uganda, Yoweri Museven imeendelea kuimarika na sasa anateleleza majukumu yake ya urais.
Wizara ya Afya ya nchi hiyo imeweka wazi kuwa baada ya Rais huyo kugundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Uviko 19, alipatiwa huduma stahiki na Sasa anaendelea vema.Museven aliomba mwenyewe kupimwa Uviko 19, baada ya kupata homa na mafua makali.
Alifanya hivyo baada ya kutoa hotuba yake Kwa Taifa Juni 7,2023 katika viwanja vya Bunge.Museveni mwenye umri wa miaka 78 aliwaambia wasaidizi wake kuwa huenda ameabukizwa Uviko 19.Taarifa ya wizara ya Afya imesisitiza kuwa Rais huyo anaendelea vizuri.
0 Comments