Timu ya Yanga imefanikiwa kujiweka pazuri kwenye kuifikia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kushinda mabao 2-0.
Yanga imepata ushindi huo kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Benjamini Mkapa baada ya kucheza na timu ya Marumo Gallants ya South Afrika.
Mchezo huo ulikuwa ni wa kwanza wa nusu fainali Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Katika mchezo huo Yanga walionekana kucheza chini ya kiwango na kusababisha kwenda mapumziko wakiwa hawajafunga wala kuonesha hatari kwa wapinzani wao.
Kipindi cha pili Marumo Gallants walirudi na mfuko Ile uke walioutumka katika kipindi cha kwanza.
Walizitumia dakika 15 za kwanza kusukuma mashambulizi langoni mwa Yanga bila mafanikio, walinzi wa Yanga walikuwa makini kuzuia mashambulizi hayo.
Aziz Ki ndie aliewainua mashabiki Yanga baada ya kufunga bao zuri akipokea pasi kutoka kwa Tuisila Kisinda kabla ya Benard Morrison kufunga bao la pili na kuwafanya kuondoka na ushindi mnono wa mabao 2-0.
Matokeo hayo yanaipa nafasi kubwa Yanga kucheza fainali kwani inahitaji sare ama ushindi na kama ni kufungwa basi itahitaji kufungwa zaidi ya hili mbili.
0 Comments