Ticker

7/recent/ticker-posts

NUKUU ZA BASHE KWENYE BAJETI YA KILIMO

*Nukuu za Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akiwasilisha Bajeti ya Kilimo Mwaka 2023/24.*

"Hadi kufikia Aprili, 2023,Bodi ya Mkonge Tanzania imesambaza miche ya Mkonge 12,633,536 katika Halmashauri 15.”

WAZIRI WA KILIMO, MHE. HUSSEIN BASHE

"Bodi ya Mkonge Tanzania kwa kushirikiana na TARI imesambaza miche bora ya mkonge 12,633,536 inayotosha kupandwa katika eneo la hekta 3,158.38 kwa wakulima wadogo.”– WAZIRI WA KILIMO, MHE. HUSSEIN BASHE

"Bodi ya Mkonge Tanzania imetoa mafunzo ya kilimo bora cha mkonge kwa wakulima wadogo 3,952 na wakulima wakubwa 17 ikilinganishwa na lengo la 8,000 na mafunzo yanaendelea.” – 

WAZIRI WA KILIMO, MHE. HUSSEIN BASHE

"Wizara kupitia TARI itakamilisha ujenzi wa maabara ya kuzalisha miche ya Mkonge kwa njia ya chupa (tissue culture) katika kituo cha TARI Mlingano.”–

WAZIRI WA KILIMO, MHE. HUSSEIN BASHE

"Katika mwaka 2023/2024 uzalishaji wa Mkonge utaongezeka kutoka tani 48,263 mwaka 2022/23 hadi tani 60,000. Ongezeko hilo litatokana na mashamba mapya yatakayoanza kuvunwa katika msimu wa 2023/24.” – 

WAZIRI WA KILIMO, MHE. HUSSEIN BASHE

"Bodi itasambaza mbegu za Mkonge 28,000,000 zitakazopandwa katika eneo la hekta 2,500; itatoa mafunzo ya kilimo bora cha Mkonge na ubora wa singa kwa wakulima wakubwa na wakulima wadogo 8,000.” – 

WAZIRI WA KILIMO, MHE. HUSSEIN BASHE

"Bodi itawawezesha wawekezaji wawili (2) kuanzisha viwanda vya kuchakata mkonge katika Mkoa wa Tanga; itanunua korona nne (4) na kuanzisha vituo viwili (2) vya kuchakata mkonge katika Halmashauri za Mkinga na Kilosa na kununua zana za kilimo kwa ajili ya uendelezaji wa mashamba ya wakulima wadogo.”–

WAZIRI WA KILIMO, MHE. HUSSEIN BASHE

"Katika mwaka 2023/24, Wizara kupitia TARI itazalisha miche 6,000,000 ya Mkonge kwenye eneo la hekta 75 itakayosambazwa kwa wakulima 150 na taasisi.” –

WAZIRI WA KILIMO, MHE. HUSSEIN BASHE

"Watafiti/wataalam 20 wa maabara ya udongo watapatiwa mafunzo ili kuiwezesha maabara hiyo kupata ithibati; wakulima na wadau 100,000 na maafisa ugani 500 watapatiwa mafunzo ya uzalishaji wa zao la Mkonge fursa zitokanazo na zao hilo na kuanzisha majaribio ya kufupisha muda wa kitalu cha  Mkonge.”– 

WAZIRI WA KILIMO, MHE. HUSSEIN BASHE

Post a Comment

0 Comments