WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu,
ameonesha masikitiko yake kufuatia mauaji ya Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Nyamongo, kilichopo wilayani Nyamongo mkoani Tarime, Dkt. Isack Sima.
Dkt. Isack ambaye alikuwa kwenye kundi la madaktari
1000 walioajiriwa na Hayati Rais Dkt. John Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya madaktari mwaka 2020, ameuawa na watu wasiojulikana kwa kumkatakata mapanga.
Mtaalamu huyo wa Afya alikutana na kadhia hiyo usiku wa Mei 3, mwaka huu akiwa njiani kurejea nyumbani kwake akitokea kazini.
Akilisemea suala hilo kupitia ukurasa wake wa twita, Waziri Ummy ameandika: very sad kumpoteza mtaalamu wetu wa Afya.Nina laani vikali tukio hili. Pole kwa familia na watumishi wote wa sekta ya afya Tarime na nchini kwa ujumla.
May his soul rest in peace!
Tunaamini vyombo vya dola vitafanikisha kupatikana kwa wahusika waliofanya kitendo hiki.
Kwa upande wake Rais wa chama cha Madaktari nchini (MAT), Dkt. Elisha Osati ameandika: Haikubaliki Dr Isack ni mmoja wa Madaktari 1000 tuliopewa na Rais Magufuli katika maadhimisho ya siku ya madaktari 2020.
Isack alikuwa tayari kuwahudumia wananchi vijijini, hivi utamwambia Dr Gani akafanye kazi Tarime. Tunaitaka mamlaka iwakamate wahusika bila kumung'unya maneno.
0 Comments