Ushindi wa 2-1 ulioipata timu ya Azam dhidi ya Simba kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara, unatajwa kuivuruga klabu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi.
Inaelezwa kuwa hali ndani ya kikosi cha Simba si nzuri na kwamba kipigo cha jana kimetoa nafasi kwa benchi la ufundi kufanya maamuzi mazito.
Hii ilikuwa nusu fainali ambayo iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka kutokana na ubora wa timu zote ambao wamekuwa wakiuonyesha kwenye Ligi Kuu msimu huu.
Azam ndiyo walikuwa wa kwanza kupachika bao kupitia kwa beki wao wa kulia Lusajo Mwaikenda, akimalizia mpira uliotemwa na kipa Ally Salim na kuipa timu yake bao la kuongoza lakini dakika ya 28 Simba walisawazisha kupitia kwa Sadio Kanoute ambaye alifunga bao safi kwa kichwa kutokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Said Ntibazonkiza'Saido' na kuzipeleka timu hizo mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
0 Comments