Katika kuhakikisha Yanga inawafunga Rivers United leo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameamua kutia shime kwenye mchezo huo kwa kununua tiketi 500.
Kimsingi homa ya mchezo huo inazidi kupanda ingawa Yanga inapewa nafasi kubwa ya kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho.
Waziri Mkuu Majaliwa amenunua tiketi 500 za mchezo huo wa mkondo wa pili wa Robo Fainali kati ya Yanga dhidi ya Rivers ya Nigeria utakaopigwa leo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu anaungana na makundi mengine ya wadau 26 waliokuwa wameshanunua tiketi hizo za mzunguko ambapo tayari jumla ya tiketi 3540 zimeshanunuliwa.
Wengine walionunua ni Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji (500), sambamba na wajumbe wa kamati ya Utendaji ya klabu hiyo Alex Ngai(100), Gerald Kihinga (100), Yanga Makaga (200).
Wengine ni Ibrahim Samuel (100), Brenden Kachenje (100), Armadillo enterprise (100), Crispo Hezron (100), Zahoro Matelephone (100), Jet &Sons (100), Bullet force security (100), Chicasa General traders (100), Tradeland commodities (100).
Wamo pia Anastacia Mbunda (100), Imtiaz Lalji (100),Tawi la Yanga Twitter Family (120), Feedlance intelligent feeding (100), Tawi la Mzumbe Alumni (200), Tosh Cargo Logistics (100), Nyambaya Cargo (100), Yanga whatsap Groups Admin (120).
Shirika la Bima la Zanzibar ZIC (100), Ramadhan Mlao (100), Tawi la Yanga Elite (500) na Tawi la Yanga Bungeni (100) na kufanya mpaka hapo Yanga kuuza tiketi 3540 kwa ununuzi wa makundi hayo ambazo ni sawa na Sh 17,700,000 milioni.
Tayari klabu hiyo mapema jana walitangaza kumalizika kwa tiketi za eneo la VPA za mchezo huo ambao endapo Yanga itaulinda ushindi wao wa awali ugenini waliposhinda kwa mabao 2-0 au kushinda tena au kutoa sare yoyote watatinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.
0 Comments