MCHEZAJI wa kimataifa wa Moroko anayekipiga kwenye timu ya PSG ya Ufaransa, Ashraf Hakimi, hana mali yoyote anayomiliki zaidi ya viatu vya soka.
Hayo yamebainika baada ya mke wake kudai talaka pamoja na kuomba mahakama kumpa mgawo sawa wa mali zote anazomiliki Hakim.
Hakimi hakukataa maombi ya talaka ya mkewe na pia alikubali mgawanyo sawa wa mali, hata hivyo mahakama ilipochunguza vizuri kwenye mali za Hakimi walikuta hamiliki kitu hata kimoja hata akaunti zake za benki hazina chochote, zaidi anamiki jezi na viatu vya soka.
Imeelezwa Hakimi alifanya hivyo Kwa Sababu alijua kama hayo mambo yatatokea na ndipo alipozikabidhi mali zake zote kwa mama yake, ambapo alizikabidhi kihalali mali na pesa zake zote kwa mama yake mzazi.
0 Comments