Aliyekuwa Mkurugenzi wa jijia la Mwanza, Sekiete Seleman
Kashfa ya uuzaji wa kiwanja bila kufuata utaratibu inatajwa kumtesa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Sikiete Yahaya Seleman ambaye ametenguliwa tangu Aprili 16, mwaka huu.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndie aliyetengua uteuzi wa Sekiete na Sababu kubwa ikitajwa kiwa ni uamuzi uliotangazwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Adam Malima Januari 13, 2023.
Mkurugenzi huyo pamoja na wakuu wa idara wanne wanadaiwa kuhusika na uuzwaji wa kiwanja na kujipatia mamilioni ya fedha.
Taarifa ya Ikulu iliyolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus haikueleza sababu.
Juzi mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima alipelema malalamiko yanayomuhusu mkurugenzi huyo kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Shilingi bilioni moja.
Wakati barua ya malalamiko ikifika Tamisemi, Malima aliagiza watumishi wanne wa jiji hilo kusimamishwa kazi Ili kupisha uchunguzi kwa tuhuma za uuzaji wa viwanja hivyo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Adam Malima
Viwanja vilivyouzwa ni namba 194 na 195 vipo mtaa wa Rwegasore jijini Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza Ijumaa Januari 13, 2023, Malima ametaja nyadhifa za watumishi wanaosimamishwa kazi kuwa ni mhasibu wa Jiji, mwanasheria, ofisa manunuzi na ofisa mipango.
Watumishi hao wa umma wanadaiwa kuuza viwanja hivyo vilivyopo mtaa wa kibiashara katikati ya jiji kwa thamani ndogo kulinganisha na bei ya soko.
Amesema walishirikiana kuuza viwanja hivyo bila kufuata utaratibu kinyume cha taratibu na maadili ya viongozi huku mkurugenzi wa jiji akidaiwa kukiuka maagizo ya kamati ya ulinzi Wilaya ya Nyamagana na ofisi ya mkuu wa mkoa.
“Kwa mamlaka yangu nimeelekeza ofisi ya katibu tawala Mkoa wa Mwanza iwasimamishe kazi watumishi wanne ambao ni wakuu wa idara kupisha uchunguzi na tunaandika barua ofisi ya Rais (Tamisemi) kwa hatua kuhusu mkurugenzi wa Jiji,” amesema Malima.
Mkuu huyo wa mkoa amesema licha ya suala la maamuzi kuachwa mikononi mwa Tamisemi, mamlaka ya mkoa unaona kuwa kiongozi huyo amekosa sifa za kuendelea kusalia mkoani humo.
Ameagiza idara ya ardhi kuangaliwa upya pamoja na watumishi hao wanne kuchunguzwa endapo wamehusika katika tukio hilo.
Makubaliano ya kikao cha Ulinzi na Usalama wilaya ya Nyamagana cha Septemba 28, 2022 kilikataza kurejesha au kufanya uwekezaji wowote wa viwanja vitano kuanzia namba 191 hadi 196 bila kamati hiyo kufahamishwa.
0 Comments