Ticker

7/recent/ticker-posts

STARS IKIFUDHU AFCON ITABEBA MILIONI 500

Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Balozi Pindi Chana imetangaza kutatoa zawadi ya tsh. Milioni 500 endapo timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itafuzu kucheza Fainali za AFCON 2023 nchini Ivory Coast. 

 “Serikali itatoa kiasi kisichopungua tsh. Milioni 500 endapo timu yetu itafuzu kushiriki Fainali za AFCON”.  Kwa sasa Taifa Stars iko nchini Misri ambapo itacheza mchezo wake dhidi ya Uganda March 24 kabla ya kurudiana March 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.



Timu ya Taifa ya Uganda inacheza mechi zake za nyumbani nchini Misri kwakuwa uwanja wake haujakidhi vigezo vya CAF.  Taifa Stas ipo Kundi F pamoja na  timu za Algeria inayeongoza kundi kwa kuwa na point 6, Niger point 2, Tanzania akishika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama moja sawa na Uganda aliye nafasi ya mwisho.

 

 Ili Tanzania ifuzu inapaswa kumaliza ikiwa katika nafasi mbili za juu katika Kundi lenye timu 4

Post a Comment

0 Comments