Kutokana na kusuasua kwenye biashara ya mawasiliano nchini, Serikali imependekeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) sasa kujikita zaidi kwenye kusimamia kampuni za mawasilino ya simu na mkongo wa Taifa na kuachana na biashara ya mawasiliano ya simu.
Hayo yamesemwa leo Machi 29,2023, Ikulu, jijini Dar es Salaam na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akipokea ripoti ya taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa mwaka 2021/2022.
0 Comments