Ticker

7/recent/ticker-posts

MBAPE AINGIA KWENYE ORODHA YA MANAHODHA WADOGO ULAYA

Kylian Mbape

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps ameripotiwa kumchagua mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe kuwa nahodha wa timu hiyo.

 Ufaransa ilikuwa haina nahodha baada ya aliyekuwa Nahodha wake mlinda mlango wa Tottenham, Hugo Lloris kutangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa Januari mwaka huu baada ya Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Qatar.

 

Mbappe alijiunga na wachezaji wenzake wa Ufaransa huko Clairefontaine Jumapili kabla ya mechi za kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Uholanzi na Ireland.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ameimarisha hadhi yake ya kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi, baada ya mabao yake muhimu kwa Ufaransa.

 

Mbappe amefunga jumla ya mabao 36 katika mechi 66 za kimataifa, ataungana na Martin Odegaard wa Norway mwenye umri wa miaka 24 kuwa mmoja wa manahodha wachanga zaidi barani Ulaya.

 

Post a Comment

0 Comments