Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta
SERIKALI kwa kushirikiana na wadau wa mchezo wa soka nchini imenunua tiketi zote za mchezo wa kesho wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za AFCON utakaoikutanisha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars dhidi ya timu ya taifa ya Uganda.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TFF hadi usiku huu tiketi zote za eneo la mzunguko ambalo lina beba zaidi ya watazamaji 30,000 zimeshanunuliwa na ndio zimetoa nafasi kwa mashabiki wengi kuingia bure.
TFF imesema milango ya uwanja wa Mkapa ya kuelekea kwenye majukwaa ya mzunguko yatafunguliwa saa sita na yatafungwa pale idadi ya mashabiki inayostahili ikifikia.
Hatua hiyo ya Serikali ambayo imechagizwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyenunua tiketi 7000 imelenga kuwaongezea hamasa wachezaji wa Stars.
Moja ya silaha kubwa inayochangia hamu ya ushindi kwenye mchezo wa soka ni mashabiki, hivyo uwepo wao kwa wingi utaibua hamasa na ari kwa wachezaji wa Taifa Stars.
Ikumbukwe kuwa Taifa Stars inahitaji matokeo ya ushindi kwenye mchezo huo Ili ijihakikishie nafasi ya kufuzu kwenye fainali za AFCON zinazotarajiwa kuchezwa mapema mwakani.
Hadi sasa Stars ina pointi nne na endapo itaifunga Uganda kama ilivyofanya kwenye mchezo wa awali uliochezwa nchini Misri itafikisha pointi sana.
0 Comments