Ticker

7/recent/ticker-posts

JWTZ KUPELEKA MSAADA WA UNGA MALAWI

  

Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda alipozungumza na waandishi wa Habari. 

Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatarajia kusafirisha misaada iliyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Jamhuri ya Malawi iliyoathiriwa na Kimbunga Freddy.

 

Akitoa ufafanuzi leo jijini Dodoma, Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema misaada hiyo inahusisha vyakula, mahema na misaada mingine ya kibinadamu.

 

"Kufuatia maafa ya kimbunga nchini Malawi, Serikali imeamua kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ili kuisaidia nchi jirani, JWTZ imepewa jukumu la kusafirisha misaada hiyo. 

 

"Tunatarajia shehena zitaondoka muda wowote kuanzia sasa, jumla ya tani 1,000 za unga wa mahindi zitasafirishwa kwenda Malawi, amesema tani 90 zitaondoka kila siku zikitokea Dodoma.

 

"Tani 60 za unga zitaondoka kila siku kutokea mkoani Iringa, mablanketi 6,000 yataondokea yakitokea Dodoma, mahema yasiyopungua 50 yataondoka yakitokea jijini Dar es Salaam," ameeleza Luteni Kanali Ilonda.

Post a Comment

0 Comments