Ticker

7/recent/ticker-posts

I AM THE STATE, KINAONESHA NCHI ILIKUWA GIZANI

Maisha ya urais ya hayati Rais wa awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli sasa yamewekwa sehemu moja, Kwenye kitabu cha I am the State.

Kitabu hicho kilichoandikwa na manguli wanna wa t tasnia ya Habari kimetoka ikiwa ni miaka miwili tangu Dkt. Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani.

Kitabu hicho kilichozibduliwa leo  kinaonyesha sura halisi  ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.

Waliokiandika ni Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu, maana halisi Kwa tafsiri ya lugha ya Kiswahili ni Mimi ndio Dola.

Maamdishi yaliyopamba Kitabu hicho yanaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato mji  alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo kuelekezwa huko kwa matakwa yake.


Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dkt. Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.

Pia kitabu hicho kimejiuliza fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uliishia wapi.

Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.

Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dkt. Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.

Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.

"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Moja ya kauli alizoppata hayati Dkt. Magufuli enzi za uhai wake ambayo imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dkt. Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.

Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya serikali.

"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.

Post a Comment

0 Comments