Ticker

7/recent/ticker-posts

KING KINYA; THE MULTI-SKILLED CARTOONIST


KATUNI za siasa au tahariri (editorial cartoons). Vibonzo vya kijamii na matukio. Drama cartoons na hadithi. King Kinya, Tanzania imepoteza kipaji bora katika tasnia ya habari.

Mahiri wa kuwasilisha ujumbe kwa michoro. Stadi wa kuvunja mbavu kwa michoro. Mwanaharakati aliyeweka hisia zake kwenye michoro. Mcheshi asilia aliyetumia kipaji chake kuuliwaza umma kupitia michoro. King Kinya, the seasoned cartoonist.

Kinya alikuwa na kichwa kinachoizunguka dunia, macho yanayoimulika tasnia, ubongo unaoitafsiri mitaa. Alijaliwa upeo mkubwa katika mambo mengi. Hii ilimfanya awe na uwanda mpana wa uwasilishaji. Sifa hiyo ni tunu kwa mwanahabari aliyebarikiwa.

Nilimfahamu Kinya kama shabiki wa kazi zake. Nilifahamiana na Kinya kama mwanachama mwenza wa tasnia. Nlishirikiana na Kinya, kama mfanyakazi mwenza. Mimi nikiwa mhariri, Kinya mchoraji. Tulihakikisha jamii inapata huduma bora katika kila kazi tuliyochapisha.

Nazikumbuka zile nyakati kila wiki tuliketi kujadili mambo ya kuilisha jamii. Kinya alikuwa package iliyokamilika. Kichwa chake kilizalisha stories. Alitambua kuwa ili uwasilishe vizuri lazima usikilize vema na utafsiri kwa usahihi. Tabia hii ilimfanya Kinya kuwa mtu maalum kwenye tasnia.

Nyakati ambazo kila mtu aliogopa kusema, Kinya alichora. Alitumia sanaa kubwa kuyasema yaliyoogopwa. Alikuwa fundi wa kucheza na codes. Usingemtia hatiani. Ungeishia tu kusonya.

Mdau wa muziki hasa Dansi. Mtu wa utani. Angekutania bila kujua mood yako. Ungedhani hayupo serious. Ukweli, Kinya aliifanya kazi yake kwa umakini hadi pumzi ya mwisho. Ni mmoja wa wachoraji wa mwanzo Tanzania kuachana na makaratasi na kutumia kompyuta. Kinya mwanateknolojia.

Zaidi ya miongo miwili ya kufahamiana na kufanya kazi pamoja, sikuwahi kumwona akigombana physically. Muungwana, mpole, na zile dread kichwani za kibishoo, lakini ungemtibua angekutia kwenye katuni.

Mara kwa mara nilishtukia kuna watu alifululiza anawachora. Ilipozidi nilimhoji, angekiri na kuacha. Yes, alitumia kipaji chake kuwakabili wagomvi wake.

Tutaonana tena Kinya. Hii ni kwetu tunaoamini kuna maisha baada ya kifo. Usiku mwema Brother.

Ndimi Luqman MALOTO

Post a Comment

0 Comments