Ticker

7/recent/ticker-posts

'IUCN IMETUONESHA TIJA YA UCHUMI WA BULUU, IMETUONDOA KWENYE UMASIKINI'

Mwenyekiti wa kikundi cha Upendo kilichopo katika kijiji cha Msarazi kata ya Bushiri wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Said Bakari.

 NA JIMMY KIANGO

"Awali hatukuwa na uelewa wa kutosha wa namna ya kujinufaisha kupitia bahari na mto Pangani uliotuzunguka, ujio wa IUCN umetusaidia kuujua uchumi wa buluu na namna ya kunufaika nao," hiyo ni kauli ya Mwenyekiti wa kikundi cha Upendo kilichopo katika kijiji cha Msarazi kata ya Bushiri wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Said Bakari.

 

Ukweli ni kwamba wakazi wa kijiji hicho pamoja na kujishughulisha na masuala ya bahari mali, lakini pia walijihusisha na kilimo cha kujikimu, lakini sasa wanaiona tija ya uwepo wa Mto Pangani.

 

Uwepo wa mto Pangani umewasogeza karibu na uchumi wa Buluu, ambao ni uchumi unaotokana na mali na shughuli za baharini.

 

Mzee Bakari anasema kabla ya kuanza kuijua thamani na matunda ya uchumi wa buluu na uwepo wa Mto Pangani, walikuwa wakinenepesha ka ana kufuga Samaki kwa mazowea tu, hali iliyokuwa ikiwafanya kutofurahia kazi yao hiyo.

 

Anasema walikuwa nab wawa moja na vifaa duni kabisa vya kufugia Samaki, kimsingi hawakuwa na uhakika na wanachokifanya kwa sababu lilikuwa ni jambo la kawaida kwa wahalifu kuingia kwenye bwawa lao la kujivulia Samaki kwa namna wanavyotaka.


 

“Tulikuwa tunafanya kazi isiyo na tija kwakweli, maana tulikuwa tunawafanyia kazi wezi na ndege, ndege walikuwa wanatusumbua sana, kiukweli hatukuwa na faida na hii kazi tofauti na ilivyo sasa.

 

“Wanapata fedha kwa sababu wanauhakika wa kuuza kilo 32,000 kipindi ambacho msimu unakuwa mzuri na hali ya msimu ikiwa mbaya wanauhakika wa kuuza kilo 22,000 za samaki na kwa mwezi mmoja wanauhakika wa kuvuna tani moja ya Samaki na kilo 50 za Kaa.”

 

Kazi kubwa inayofanywa na kikundi hicho ni kunenepesha Kaa, ambao wanawanunua kutoka kwa wavuvi kwa gharama ya shilingi 5000 kwa kilo moja na wanachokifanya ni kuhakikisha kaa wanaemnunua kutoka mvuvi hakosi uzito wa gram 350 moaka 400.

 

Mzee Bakari anasema wanatumia wiki tatu mpaka nne kunenepesha Kaa ili kuwaingiza sokoni, huku wakitumia wiki 20 hadi 24 kufuga Samaki na kuwaingiza sokoni na kutokana na kuwa na mabwawa matatu sasa wanauhakika wa kuvua Samaki kwa wastani wat ani moja kila mwezi.  

 

Akizungumzia ujio wa Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Uasilia (IUCN), Mzee Bakari anasema Shirika hilo limeanza kuwafadhili kati yam waka 2023/24 na kabla ya ujio wao hali haikuwa nzuri na hata tija haikuwepo..

 

Baada ya IUCN kuja sasa hali imekuwa ni nzuri, wamejenga mabwawa ya kisasawameweka mlinzi Pamoja na kuweka kamera kwenye eneo lote la mradi.

 

“Awamu ya kwanza IUCN wametupatia kiasi cha shilingi milioni 32, ambayo tumeitumia kujenga mabwawa, kuweka kamera, fensi, tenki za maji,mashine ya kujazia maji na bomba za kuingizia maji.

 

“Katika awamu ya pili milioni IUCN walitupatia kiasi cha shilingi milioni 16, fedha hizo tumezitumia kununua nyavu za kufunika mabwawa ili kuwakinga Samaki na ndege, kununua mitumbwi kwa ajili ya kuwawezesha wavuvi wakavue Kaa na kuja kuwauzia kwa urahisi.

 

Mzee Bakari, amesema changamoto kubwa inayowakabili ni chakula cha samaki, ni ghali sana na upatikanaji wake unasumbua, alitaja chakula hicho kuwa ni  Karanga au mashudu ya alizeti, mahindi, maharage ya soya na madini.

 

Kilo ya chakula cha samaki ni tsh 3,600, usafiri wa kusafirisha kilo 25 za chakula hicho ni tsh 16,000 kutoka Dar es Salaam, mpaka Pangani mjini, na kutoka Pangani mjini mpaka kituoni inawagharimu shilingi 3000 za usafiri.

 

“Tunaiomba serikali iangalie namna ya kutupa ruzuku ya vyakula vya Samaki au itusaidie mashine za kuzalisha chakula hicho ili tuwe tunatengeneza wenyewe, kiukweli vyakula vya Samaki ni ghali sana,”alisema.

 

Pamoja na kufuga Samaki na kunenepesha kaa, kikundi hicho pia kinashiriki moja kwa moja katika ulinzi wa mazingira, ambapo kauli mbiu yao ni 'Asiyependa mikoko, samaki kuwapoteza, fukwe kuzihariju, joto kuongezeka na majabali kutuvamia." 

Post a Comment

0 Comments