NA MWANDISHI WETU
Benki ya KCB Tanzania, imerejesha kwa jamii kiasi cha Shilingi milioni 30 ikiwa ni mchango wake wa kufanikisha sherehe ya shukrani ya shule za Marian.
Agosti 31,2024 Taasisi ya Marian iliandaa sherehe maalum za shukurani zilizohusisha shughuli mbalimbali zikiwemo za mbio za pole na Ibada ya shukrani.
Mgeni rasmi wa sherehe hizo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kanda wa KCB Group na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Tanzania, Cosmas Kimario aliipongeza Taasisi za Marian kwa mafanikio makubwa waliyoyafikia kielimu, kijamii, na kiuchumi.
Kimario alisisitiza kuwa tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka 1997, zimeonyesha dhamira thabiti ya kutoa elimu bora na kuzalisha wahitimu wenye mchango mkubwa katika jamii na tija kazini.
Alisema Marian imekuwa ikikua mwaka hadi mwaka, ambapo imetoka kuwa na shule moja ya sekondari ya Wanawake ‘Marian Girls Secondary School’, hadi kuwa na shule tatu za Sekondari, Zahanati, Hoteli, na Chuo Kikuu (Marian University), kilichoanzishwa mwaka 2014.
“Mafanikio haya yameleta mabadiliko chanya katika elimu, jamii, na uchumi wa taifa, wahitimu wa Marian Schools wameiva kielimu na kinidhamu, wakitoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa.”
Kwa upande wake Meneja wa Shule za Marian, Fr. Valentine Bayo, alitoa historia fupi ya Taasisi za Marian, akisema: "Mnamo mwaka 1991 alitumwa hapa na wakubwa wake kutoka Shirika la Roho Mtakatifu (Holy Ghost Fathers) kama Padre kijana kwa kazi ya uinjilishaji.
“Kutokana na hali ya uduni wa eneo hili ambalo lilikuwa limesahaulika, tulianzisha juhudi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuanzisha shule za chekechea na ufundi. “Hatimaye, juhudi hizi zilipelekea kujengwa shule ya sekondari ya wasichana ya Marian mnamo mwaka 1997. Tangu kuanzishwa kwake, shule hii imekuwa kielelezo cha mafanikio nchi nzima na kupelekea uanzishwaji wa taasisi nyingine za Marian kama zifuatazo:"
1. Marian Pre and Primary School
2. Marian Boys Secondary School - Kerege
3. Marian Boys Secondary School - Mlingotini
4. Marian Mater Dei Girls Secondary School
5. Stella Maris Hotel
6. Marian Aggregates and Concretes Ltd
7. Marian Farms
8. Marian Pre and Primary School
9. Marian Boys Secondary School - Kerege
10. Marian Boys Secondary School - Mlingotini
11. Marian Mater Dei Girls Secondary School
12. Stella Maris Hotel
13. Marian Aggregates and Concretes Ltd
14. Marian Farms
15. Marian University
USHIRIKIANO KATI YA KCB BANK NA TAASISI ZA MARIAN
Kati ya mwaka 2021 na 2024, Benki ya KCB imewekeza katika miradi mbalimbali ya Taasisi za Marian, ikiwa ni pamoja na ukarabati wa shule za Marian Girls na Marian Primary, ujenzi wa majengo ya ghorofa sita kwa ajili ya madarasa na Mabweni za Marian Boys School, na kuchangia baadhi ya gharama za uendeshaji wa taasisi hizi.
Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Askofu Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu Zanzibar, Agustine Shao, Mkuu wa Shirika la Holy Ghost, Shauri Selenda, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Meneja na Mwanzilishi wa Taasisi za Marian, Fr. Valentine Bayo, viongozi na wafanyakazi wa KCB Bank,Mapadri wa Shirika la Roho Mtakatifu; wenyeviti wa bodi za Taasisi za Marian, pamoja na wazazi, wanafunzi, na wafanyakazi wa taasisi hizo.
Tangu kuanzishwa kwake, shule hii imekuwa kielelezo cha mafanikio nchi nzima na kupelekea uanzishwaji wa taasisi nyingine za Marian.
Sherehe hiyo iliadhimishwa kwa shangwe kubwa, ikionyesha umoja na mshikamano kati ya Taasisi za Marian na wadau wake, wakiwemo KCB Bank, katika kukuza maendeleo ya elimu na jamii kwa ujumla.
Fr. Valentine Bayo, Meneja wa Shule za Marian, alitoa historia fupi ya Taasisi za Marian, akisema: "Mnamo mwaka 1991 nilitumwa hapa na wakubwa wangu wa Shirika la Roho Mtakatifu (Holy Ghost Fathers) kama padre kijana kwa kazi ya uinjilishaji.
Kutokana na hali ya uduni wa eneo hili ambalo lilikuwa limesahaulika, tulianzisha juhudi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuanzisha shule za chekechea na ufundi. Hatimaye, juhudi hizi zilipelekea kujengwa shule ya sekondari ya wasichana ya Marian mnamo mwaka 1997.
0 Comments