Ticker

7/recent/ticker-posts

TANZANIA YASITISHA SAFARI ZA NDEGE ZA KQ

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesitisha safari za ndege za Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kati ya Dar es Salaam na Nairobi kuanzia Januari 22 mwaka huu. 

TCAA imesema uamuzi huo ni matokeo hatua iliyochukuliwa na mamlaka za usimamizi wa anga ya Kenya kukataa ombi la kibali cha safari kwa ndege ya mizigo ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) lililotaka kufanya safari kati ya Nairobi na mataifa mengine. 

Mkurugenzi wa TCAA, Hamza Johari amesema uamuzi uliochukuliwa na Kenya ni kinyume cha kifungu namba nne cha mkataba wa ushirikiano wa huduma za anga kati ya Kenya na Tanzania ulioingiwa Novemba 24, 2016.

Post a Comment

0 Comments