Ticker

7/recent/ticker-posts

ONANA AWASHANGAA WANAOMTUNGIA UONGO AFCON

"Ninayo mengi sana ya kuongea kwa sasa ila nimeamua kukaa kimya kwa heshima ya Timu yangu ya Taifa na mpira wa Afrika kwa ujumla.. ila kwa ufupi waandishi wa kiafrika wanapaswa wasifuate mkumbo wa waandishi wa Ulaya kuhusu namna wanavyonidhalilisha.

"Ukweli ambao waandishi wengi walikuwa hawaujui kuhusu mimi jana ni kwamba Kocha alishaniambia mapema nikicheza mechi dhidi ya Spurs hatonipanga katika mchezo wa kwanza wa AFCON na nililiheshimu hilo kwasababu mwenye kipaji cha kukaa golini kwetu Cameroon sio mimi pekee, wapo vijana kama Ondoa na ndio nilitamani wapangwe katika mchezo ule endapo nikikosekana na ikawa hivyo."  

"Mtu unachukua Picha nikiwa Koridoni naongea mambo ya kimpira na Ma-Legend kadhaa wa Soka la Arika halafu unaweka Mitandaoni na kusema nilikuwa nimekasirika kisa sijapangwa kwenye mchezo.. hii sio sawa.. lakini nishawazoea.. 

"Ninachokijua mimi nipo kwa ajili ya kulipambania Taifa langu la Cameroon kutwaa Ubingwa wa AFCON na ndio walioniamini na kuniita hapa hayo mengine ngoja niyakalie kimya kwasasa," hizo ni kauli za Melinda mlango wa Cameroon, André Onana kuhusu Taarifa za uongo anazopakaziwa Mtandaoni kabla na baada ya Mchezo wa Jana

Post a Comment

0 Comments