Ticker

7/recent/ticker-posts

TANZANIA NA KENYA ZAMALIZA TOFAUTI ZAO ANGANI

Tanzania na Kenya zimeondoa zuio la usafiri wa anga lililokuwa limewekwa kwa ndege za kila nchi. 

Awali, Tanzania ilitangaza kusitisha safari za ndege za Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kati ya Dar es Salaam na Nairobi kuanzia Januari 22 mwaka huu, hatua iliyokuja kufuatia mamlaka ya anga ya Kenya kukataa ombi la kibali kwa ndege ya mizigo ya Tanzania kufanya safari kati ya Nairobi na nchi nyingine.

 Taarifa ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema Kenya imetoa kibali hicho kwa ndege ya mizigo ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kuanzia Januari 16 mwaka huu. Kufuatia uamuzi huo, Tanzania nayo imeondoa zuio ililokuwa imeliweka kwa ndege za Kenya.

Post a Comment

0 Comments