Ticker

7/recent/ticker-posts

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI ONGEZEKO LA WATALII AFRIKA

Hatua ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya filamu ya Royal Tour imeipaisha Tanzania kwenye ongezeko la Watalii Afrika, ambapo sasa inashika nafasi ya pili nyuma ya Ethiopia.

Kidunia Tanzania imepaa hadi kuwa nafasi ya 10 huku idadi ya Watalii ikiongezeka kwa asilimia 19 hadi kufikia Septemba 2023.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Novemba 30,2023 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani iitwayo " World Tourism Barometer" utalii wa  Ethiopia umekuwa kwa asilimia 26.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa idadi hiyo inalinganishwa na idadi ya juu iliyopata kufikiwa kabla ya janga la Uviko-19 mwaka 2019.

Katika kipengele cha mapato kwenye sekta ya Utalii, Tanzania imekuwa ya 10 duniani na ya tatu Afrika ikiwa nyuma ya Mauritius na Morocco.


Kipengele hicho kinagusa ongezeko la  kiwango kikubwa cha mapato ya nchi  ikilinganishwa na mwaka 2019, ambapo ripoti hiyo inaonesha mapato ya Tanzania yameongezeka kwa asilimia 26.

Qatar ndio inaiongoza Dunia kwa idadi ya watalii ikifuatiwa na Saudi Arabia, Andora na  Albania.

Hali imeendelea kuwa ya kusuasua kwa Mataifa makubwa ya Ulaya na Marekani kurejea kwenye hali yake ya kawaida waliyokuwa nayo kabla ya janga la Uviko-19.

Post a Comment

0 Comments