Ticker

7/recent/ticker-posts

KIKONGWE CHA MIAKA 110 CHAUA MKE BAADA YA KUNYIMWA UNYUMBA

Polisi wa wilaya ya Ntungamo nchini Uganda, wanamshikilia kikongwe Dominic Babiiha mwenye umri wa miaka 110 kwa tuhuma za kumuua  mkewe mwenye umri wa miaka 109 kwa kosa la kumnyima unyumba.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa mkoa wa Rwizi, Samson Kasasira, Mzee Babiiha anatuhumiwa kumuua mkewe Costansio Bakasisa kwa kitu kizoto Jumamosi ya Desemba 16,2023 majira ya saa moja asubuhi nyumbani kwao eneo la Kahunga.

Taarifa  zinaeleza kuwa wazee hao ambao ni wakulima wamekua wakiishi pamoja na wajukuu zao.

Polisi wamesema mkewe alikataa kumpa tendo la ndoa sababu alikua akijisikia vibaya, ambapo licha ya hayo bibi huyo aliendelea kulazimishwa tendo hilo ambapo aliamu kwenda kulala chumba cha wajukuu zake.

Mzee huyo aliamua kuchukua mundu na kumuamuru atoke nje ya chumba, baada ya bibi kugoma, babu aliingia kwenye chumba hicho na kumshambulia na mundu mfululizo huku wajukuu wakikimbia nje kuomba msaada.

Kikongwe huyo anatarajia kufikishwa Mahakamani ili kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.

Post a Comment

0 Comments