Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS DKT. MWINGI ATOA MIKOPO ISIYO NA RIBA YA BILIONI 21 NA KUZALISHA AJIRA MPYA 75,000

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kipindi cha Miaka Mitatu ya uongozi wake amefanikiwa kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya Bilioni 21 na kuzalisha ajira mpya zaidi 75,000.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchuni (ZEEA) Juma Burhan Mohammed amesema kwamba miaka Mitatu ya Rais Dk.Mwinyi imekuwa miaka ya mafanikio kutokana na wananchi kunufaika na mikopo isiyo na riba ambayo imewainua katika shughuli wanazofanya.

"Kwanza nimpongeze Rais Dk.Mwinyi kwa kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake, hakika miaka hii imekuwa miaka ya mafanikio makubwa mikopo yenye thamani ya bilioni 21 imetolewa Unguja na Pemba na kuzalisha ajira zaidi ya 75,000," amesema Juma Burhan Mohammed.


Post a Comment

0 Comments