Ticker

7/recent/ticker-posts

WAKILI MWABUKUSI APONDA VYAMA VYA UPINZANI

Upinzani na CCM hawana tofauti, kitendo cha kutaka kuingia kwenye uchaguzi bila katiba mpya ni kwa sababu ya maslahi binafsi na sio maslahi ya Taifa, ndio maana kuna chawa wa chama tawala na huku upinzani nako kuna machawa.

Alisema kwenye upinzani, hakuna mtu yuko tayari kumwambia kiongozi wake kwamba anayoyafanya hayako sawa. "Hatuna hata mgambo lakini nakuhakikishia sisi wapinzani ni wabaya kuliko hawa walioko madarakani.

"Tunaogopana kuambiana ukweli, sisi na CCM hatuna tofauti kabisa,najiuliza kwanini wapinzani tunashindwa kuonyesha msimamo? kwanini twende kushiriki uchaguzi bila Katiba mpya? "Nilishasema kuna biashara ya demokrasia inafanyika hapa nchini."

Post a Comment

0 Comments