Ticker

7/recent/ticker-posts

TANZANIA NA INDIA KUSHIRIKIANA KWENYE USALAMA WA MITANDAO

Tanzania na India  zimetia saini hati za makubaliano 14 na mkataba mmoja, hati 10 kati ya hizo zimehusisha taasisi za serikali na hati tano ni kwa ajili ya  sekta binafsi.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo Oktoba 9, 2023 katika ziara ya kikazi ya Rais Samia Suluhu Hassan anayoendelea kuifanya nchini India. 

Rais Samia ameishukuru India kwa kuanzisha kampasi ya kwanza ya chuo cha IIT nje ya India chenye hadhi ya juu katika masuala ya teknolojia visiwani Zanzibar kitakachowanufaisha wanafunzi mbalimbali. 

Pamoja na mambo mengine Rais Samia ameitumia ziara hiyo kujadili masuala ya usalama wa mitandao, kushirikisha vijana hasa kupitia vyuo vya ufundi, kutoa mafunzo kwa wahandisi wa madini, kushirikiana kwenye kilimo na miradi ya maji.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania na India zimekubaliana kukuza uhusiano wao wa kihistoria  kwa kiwango cha ushirika wa Kimkakati.

Post a Comment

0 Comments