Ticker

7/recent/ticker-posts

PALESTINA YATISHIA KUUA MATEKA WAKE KUTOKA ISRAEL

Kundi la wanamgambo wa Hamas limetishia kuwaua mateka wa Israel walio chini yao iwapo nchi hiyo itarusha makombora yake katika ar

BBC imeripoti kuwa Hamas imesema kitendo cha Israel kuwalenga raia katika eneo la Gaza kinachochea hasira zaidi na kuonya kwamba kila wakati Israel inapopiga eneo hilo, Hamas wataua mateka mmoja.

"Tunatangaza kwamba kila shambulio linanalolenga watu wetu majumbani mwao, litafidiwa kwa kuuawa kwa mateka wa raia wa adui zetu," amesema Abu Obeida, Msemaji wa Qassam, katika ujumbe wa sauti uliotolewa jana Jumatatu, huku akigusia kwamba mauaji hayo yatarushwa kwa njia ya sauti na video.


Muda mfupi baada ya kauli ya Obeida, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alionya kwamba picha za uharibifu na zilizosambaa kutoka ngome za wanamgambo wa Hamas, ni mwanzo wa kile wanachotegemea kukifanya.

Wakati haya yakitokea, imeelezwa kuwa jumla ya vifo kutokana na mashambulizi hayo kwa pande zote mbili, imefikia watu 1,500; huku Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu Akitangaza kuwa nchi yake iko kwenye vita ambavyo haikuvianzisha.

Netanyahu amesisitiza kuwa Hamas ijiandae kulipa gharama ambayo “haitasahaulika maishani mwao” na kwa maadui wote wa Israel, na kwamba “lazima Israel itashinda vita hivyo na ikishinda basi dunia nzima itashinda.”

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amesema anasikitishwa na amri ya Israel ya kuzingira Gaza na kukata umeme, chakula na mafuta katika eneo hilo lenye wakazi wengi.


Pia amelaani mashambulizi ya makombora ya hospitali na makazi katika Ukanda wa Gaza, akiomba Umoja wa Mataifa uruhusiwe kuingia kutoa misaada ya kibinadamu.

Jana, Guterres amezungumza na vyombo vya habari baada ya kukutana na viongozi wakuu, akilaani kitendo cha Hamas kuwateka mateka raia na wanajeshi, pia ameelezea wasiwasi wake juu ya ripoti za zaidi ya Wapalestina 500 waliouawa huko Gaza.

Ameionya Israel kwamba operesheni za kijeshi lazima zifanywe kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu.

Post a Comment

0 Comments