Ticker

7/recent/ticker-posts

WAFANYAKAZI KIUTA WAPINGA KIWANDA KUUZWA

BAADHI ya wafanyakazi wa kiwanda cha Uchapaji cha Taifa (KIUTA) kilichopo barabara Nyerere jijini Dar es salaam wameandamana leo Septemba 11,2023 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni  kuuzwa kinyemela kwa kiwanda hicho.

Taarifa ilizozipata Afrinews Swahili zimeeleza kuwa kiwanda hicho kimeuzwa  kwa Kampuni ya  SuperDoll kwa thamani ya Sh. Bil 10.

Wanaotajwa kuhusika na uuzaji huo ni baadhi ya viongozi wa bodi ya kiwanda hicho huku kukiwa hakuna ridhaa ya wamiliki.

Wahusika  wanaodaiwa kuuza Kiwanda hicho ni Mwenyekiti wa Bodi Patrick Nyundo na Mjumbe wa Bodi Pastory Kyomba. Kiwanda kimeuzwa bila ridhaa ya mamlaka husika.






Post a Comment

0 Comments