TANZANIA kwa mara ya kwanza inaingia kwenye historia ya kuandaa michuano mikubwa ya soka Barani Afrika kwa ngazi ya Taifa AFCON.
Leo Septemba 27,2023 nchi hiyo pamoja na nchi mbili za ukanda wa Afrika Mashariki, Kenya na Uganda zimepewa nafasi ya kuandaa fainali za michuano hiyo ya AFCON zitakazochezwa mwaka 2027.
Tayari Shirikisho la Soka barani Afrika CAF limethibitisha rasmi kuwa mataifa hayo ya Tanzania, Kenya na Uganda yataandaa michuano hiyo kutokana na kupigiwa kura nyingi.
Upigaji huo wa kura umefanyika Cairo nchini Misri.
Hatua hiyo inamaanisha kuwa uwanja wa Benjamin William Mkapa na ule waAmaan uliopo Zanzibar vitatumika katika michezo ya mashindano hayo.
0 Comments