Ticker

7/recent/ticker-posts

​URUSI YAFURAHISHWA NA KEPTENI IBRAHIM TRAORE

Urusi na nchi washirika wake kibiashara (BRICS) wamefurahishwa na Rais mdogo Kuliko wote duniani, Ibrahim TRAORE na kuamua kumpa tuzo ya heshima. 

Tangu aingie madarakani Septemba 2022, Kwa mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso, Traore ameifanya Urusi  ifungue Ubalozi nchini  Burkina  Faso.

Aidha ameviondoa vikosi vya Ufaransa huko Burkina Faso na Amezuia usafirishaji wa Uranium kwenda Ufaransa na Marekani.

Ibrahim Traore ni  kiongozi mpya wa kijeshi nchini humo na pia amekuwa 

Mkuu mpya wa jeshi la Burkina Faso.

Kapteni Ibrahim Traore, ndiye kiongozi mdogo zaidi wa eneo hilo na mwanajeshi mkakamavu ambaye amekuwa akikosoa zaidi  mikakati isiyofanikiwa ya mtangulizi wake dhidi ya kundi la  Islamic State na wanamgambo wa al-Qaeda.


Kapteni Traore alimpindua Luteni Kanali Paul-Henri Damiba  Septemba 30,2022 ikiwa ni mapinduzi ya pili ya kijeshi kwa mwaka huo. Mapinduzi hayo yanatajwa kupunguza kasi ya kuirejesha nchi hiyo kwenye utawala wa kiraia.

Traore, alianza kazi yake ya kijeshi mwaka 2009 na ametumikia vikosi mbalimbali vya Mashariki na Kaskazini mwa Burkina Faso.

Alikuwa miongoni mwa kundi la wanajeshi waliounga mkono mapinduzi ya Damiba ya Januari 24, 2022 dhidi ya Rais aliyechaguliwa kidemokrasia Roch Marc Kabore.

Hata hivyo, miezi minane baadaye, migawanyiko iliibuka katika serikali kuu inayojulikana kama Vuguvugu la Patriotic for Preservation and Restoration (MPSR).

Mbinu mbalimbali zilizotumiwa na utawala wa muda wa kijeshi wa Kanali Damiba,  ikiwa ni pamoja na mageuzi kwa jeshi linalounga mkono jeshi la kujilinda, uteuzi wa magavana wa kijeshi katika maeneo yenye ghasia na kuongezeka kwa operesheni kaskazini na mashariki  zimeshindwa kuzuia mashambulizi mabaya ya wanamgambo dhidi ya raia na usalama wao.


Kulingana na wachambuzi wa data za migogoro ACLED Info, Burkina Faso ilichukua nafasi ya nchi jirani ya Mali kama kitovu cha ghasia za wanamgambo mwaka huu jana na kusababisha maandamano ya kumtaka Damiba ajiuzulu.

Wakati mapinduzi ya kijeshi yalikuwa ya kushangaza, jeshi la Burkina Faso kwa muda mrefu limekuwa na hali ya kutoaminiana na kutoridhika tangu mapinduzi yaliyoshindwa ya mwaka 2015 ambayo yalisababisha kusambaratishwa kwa jeshi la wasomi.

Aidha maadili ya vikosi vya usalama yameathiriwa zaidi na mashambulizi ya mara kwa mara ya waasi na mazingira duni ya kazi, hasa katika maeneo ya mipakani yenye hali tete.

Mara baada ya kunyakua madaraka kwa Capt Traore, vita vya maneno vilianza kati ya kikundi chake na kile cha Damiba na kuzua hofu ya mzozo mkali wa madaraka.

Kujiuzulu kwa Damiba Oktoba 2,2022  kulimweka Traore kuwa msimamizi wa jeshi lililogawanyika linalojitahidi kukabiliana na uasi wa kikatili ambao unaendelea kuyumbisha sehemu kubwa za Burkina Faso na Sahel.

Kapteni Traore alizaliwa mwaka 1988 na alianza elimu yake Bondokuy, mji wa jimbo la magharibi la Mouhoun.

Kisha akahamia jiji la pili la nchi hiyo, Bobo-Dioulasso, kwa ajili ya elimu yake ya shule ya Sekondari.

Akiwa katika shule, Traore alielezewa kuwa ni mwenye haya na msiri mkubwa na mwenye akili nyingi sana".

Chama cha Muslim Pupils and Students of Burkina (AEEMB) kilisema pia alikuwa ni  kijana mtulivu sana.

Mwaka 2006, alijiunga na Chuo Kikuu cha Joseph Ki-Zerbo katika mji mkuu, Ouagadougou ambapo alihitimu kwa heshima ya juu, kisha akapata mafunzo katika Chuo cha Georges Namoano katika mji wa kusini-kati wa Po.

Traore alijiunga na jeshi mwaka wa 2009 na kupata cheo chake cha kwanza miaka miwili baada ya kuhitimu mafunzo ya awali. Pia alichukua mafunzo ya upigaji risasi nchini Morocco.

Alihamishiwa katika kikosi cha silaha huko Kaya katika Mkoa wa Kati-Kaskazini.

Alipandishwa cheo hadi kuwa Luteni mwaka 2014.

Traore baadaye alihudumu katika ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali - unaojulikana kwa ufupi kwa lugha ya Kifaransa kuwa Minusma na inasemekana alikuwa miongoni mwa walinda amani ambao walionyesha ushujaa wa  kukabiliana na shambulio tata la wanamgambo katika Mkoa wa Timbuktu kaskazini mwa Aprili 2018. .

Mwaka 2019, Traore alishiriki katika operesheni ya kijeshi iliyopewa jina la "Otapuanu" mashariki mwa Burkina Faso iliosabbaisha utulivu kwa miezi saba. Pia alifanya kazi  katika kikosi cha MarkoyeKaskazini mwa Mkoa wa Sahel na kushiriki katika operesheni kadhaa kaskazini.

Mwaka 2020, alipandishwa cheo na kuwa kapteni.

Tangu Machi mwaka jana, Traore amekuwa mkuu wa kikosi cha silaha kilichoko Kaya.

Kwa maneno yake mwenyewe aliwahi kusema kuwa 

‘’Makubaliano yetu kwa pamoja yamesalitiwa na kiongozi wetu  Luteni Kanalii Paul Henri Damiba. Kuzorota kwa hali ya usalama kumetufanya kuchukua hatua ,makubaliano yetu ya awali yametupiliwa mbali kutokana na tamaa za kisiasa’’.- aliyasema hayo  Septemba 30 2022 alipoongea na na kituo cha Habari cha serikali cha  RTB TV.

’Sikuamua kuchukua  madaraka, nilichaguliwa. Ni hali ambayo imekuwa ikitokota kwa wiki tatu sasa. Nilikaa kwa takriban wiki moja mjini Ouagadougou nikijadiliana naye. Lakini hakuna lililojiri. Na raia waliona namna mambo yalivyokwenda…tulipendekeza suluhu chungu nzima na nikaelewa mwishoni kuwa tunacheza mchezo wa siasa badala ya kile tulichokubaliana,’’.- aliyasema haya Oktoba 2, 2022 katika idhaa ya VOA ya Ufaransa.

‘’Najua kwamba Ufaransa haiwezi kuingilia moja kwa moja masuala yetu ya ndani. Iwapo tuna washirika wengine wanaoweza kutuunga mkono , sio Urusi.  Wamarekani ni washirika wetu lakini pia tunaweza kushirikiana na Urusi, hivyo basi sio kuhusu Ufaransa au tatizo la Urusi na Wagner’’. Oktoba 2 2022 katika chombo cha Habari cha France 24.

‘’Najua mimi nina umri mdogo sana zaidi ya wengi wenu hapa. Hatukutaka kilichotokea lakini hatukuwa na namna, kwa siku chache zilizopita , tumeusumbua usingizi wenu, tumesumbua usingizi wa wakaazi wa Ouaga kwa milio ya risasi. Hatukutaka hilo kufanyika, lakini haya ndio maisha…katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, lazima tufanye kile ambacho kilipaswa kufanywa katika kipindi cha miezi minane iliyopita…kila kitu ni dharura’’. -Oktoba 2 2022 akizungumza na maafisa wa wizara mbalimbali.

Kile ambacho wengine wanasema

‘’Ni miongoni mwa maafisa wenye umri mdogo wa jeshi ambao walihusika katika mapinduzi ya Rais Roch Marc Christian Kabore na kumuweka uongozini Damiba, lakini hivi sasa amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya mpito’’, gazeti la Ufaransa la Jeune Afrique lilisema Septemba 30 2022.

"Ibrahim Traore  amechukua uogozi wa nchi, kama  Thomas Sankar  mwenye umri wa miaka 34 kama yeye baada ya mapinduzi ya kijeshi. Je ipi hatma ya Burkina Faso’’.

‘’Traore yuko karibu na wanajeshi wenzake  na ni jasiri.

Post a Comment

0 Comments