Ticker

7/recent/ticker-posts

​HAKIMU WA KIUME AJIFANYA MWANAMKE ILI AMSAIDIE MPENZI WAKE KUFANYA MITIHANI

Msajili Mkuu wa Mahakama nchini Uganda amemfuta kazi Hakimu mmoja  kutoka utumishi wa mahakama baada ya kukamatwa kwa kujifanya mwanamke ili kufanya mitihani ya sheria kwa niaba ya mpenzi wake.

Ammaari Musa Semwogerere aliteuliwa kuwa Afisa wa Mahakama mwezi uliopita na Tume ya Huduma za Mahakama kwenye nafasi ya Hakimu Daraja la Kwanza kwa muda wa majaribio.

Jumatano ya wiki iliyopita, Semwogerere alikamatwa akiwa anaendelea kufanya mtihani kwa niaba ya mmoja wa wanafunzi wa kozi ya sheria anayejulikana kwa jina la Irene Mutonyi, ambaye inasemekana ni mpenzi wake, katika Kituo cha Maendeleo ya Sheria huko mji wa Lira, kaskazini mwa Uganda.Hakimu huyo alikamatwa na siku ya Ijumaa alishtakiwa kwa makosa mawili ya kutoa hati ya uongo na kosa moja la kujifanya mtu mwingine.


Mahakama iliyotoa taarifa baada ya tukio hilo ilisema uteuzi wake mpya umefutwa.Msajili Mkuu wa Mahakama, Sarah Langa Siu, alisema miongoni mwa kanuni kuu katika Kanuni ya Maadili kwa maafisa wa mahakama ni uwazi, akikitaja kama msingi muhimu kwa utendaji mzuri wa ofisi za mahakama.

Kwa sasa, Semwogerere amewekwa rumande hadi Agosti 3 mwaka huu, atakapofikishwa tena mahalamani

Post a Comment

0 Comments