Ticker

7/recent/ticker-posts

MAX NZENGELI KIVULI KINACHOTEMBEA UWANJANI

Na. Jimmy Kiango -Afrinews DSM

Max Mpia Nzengeli,  kijana mdogo kabisa aliyezaliwa Januari 30,2000 kwenye mji wa Mushie nchini DRC.

Hana tattoo, kiduku wala hajajichubua ngozi, yuko real, bila shaka haamini katika kuyafanya hayo.

Matendo yake yanaonesha ni mwenye nidhamu ya hali ya juu na hofu ya Mungu.

Anachomekea muda wote awapo kazini (uwanjani) analifanya hilo kwa kumaanisha.

Nzengeli amezaliwa kufanya kitu kimoja tu, nacho ni kuwapa burudani ya soka mashabiki wake.

Amezaliwa kucheza mpira wa kisasa na wa zamani, haongei mdomoni, anaitumia miguu yake kuzungumza.

Nzengeli amewalazimisha   mashabiki wengi wa soka Tanzania hasa wale wa Yanga kumsahau Mayele.

Nzengeli hakabiki ndani ya uwanja kwa sababu huwezi jua utampata wapi ni kama kivuli, unakiona ila huwezi kukikamata.

Kila kwenye njia inayopita mpira yupo, nyuma utamkuta, mbele utamkuta, kushoto yupo, kulia kajaa, katikati ndio usiseme anachafua balaa.

Hakati tamaa na hachoki. Amekuja Tanzania kucheza soka na kuvuta mkwanja, hakuja kunyoa viduku. Nzengeli, atawasumbua wengi hasa Ligi Kuu.



Post a Comment

0 Comments